Nyumbani › Agano la Kale › Zaburi
Zaburi 140
Maandiko: Biblia Takatifu, Unlocked Literal Bible, © 2019, CC BY-SA 4.0. Vichwa, utangulizi na picha: Imago Biblia.
Picha za sura hii zinakuja hivi karibuni. Kwa sasa, haya ni maandiko kamili.
Yahwe, uniokoe dhidi ya waovu; unikinge dhidi ya watu wenye vurugu.
Wao wanapanga uovu mioyoni mwao; wanasababisha mapigano kila siku.
Ndimi zao zinajeruhi kama nyoka; sumu ya fira imo midomoni mwao. Selah
Ee Yahwe, unilinde dhidi ya mikono ya waovu; unikinge na vurugu za watu wanaopanga kuniangusha.
Wenye majivuno wameweka mtego kwa ajili yangu; wameeneza nyavu; wameweka kitanzi kwa ajili yangu. Selah
Nilimwambia Yahwe, “Wewe ni Mungu wangu; usikie kilio changu unihurumie.”
Ee Yahwe, Bwana wangu, wewe ni mwenye nguvu uwezaye kuniokoa; hunifunika ngao kichwa changu siku ya vita.
Ee Yahwe, usiyatimize matakwa ya waovu; usiruhusu njama zao kufanikiwa. Selah
Wale wanao nizunguka huinua vichwa vyao; madhara ya midomo yao wenyewe na yawafunike.
Makaa ya moto na yawaangukie; uwatupe motoni, kwenye shimo refu, wasiweze kuinuka tena.
Watu wenye ndimi na wasifanywe salama juu ya nchi; na uovu umuwinde kumpiga mtu mwenye vurugu mpaka afe.
Ninajua kuwa Yahwe atahukumu kwa haki walioteswa, na kuwa atawapa haki wahitaji.
Hakika watu wenye haki watalishukuru jina lako; watu wanyoofu wataishi uweponi mwako.