Nyumbani › Agano la Kale › Zaburi
Zaburi 82
Maandiko: Biblia Takatifu, Unlocked Literal Bible, © 2019, CC BY-SA 4.0. Vichwa, utangulizi na picha: Imago Biblia.
Picha za sura hii zinakuja hivi karibuni. Kwa sasa, haya ni maandiko kamili.
Mungu amesimama katika kusanyiko la mbinguni; katikati ya miungu anahukumu.
Hata lini mtahukumu bila haki na kuonesha upendeleo kwa waovu? Selah
Wateteeni maskini na yatima; dumisheni haki kwa aliyetaabishwa na fukara.
Muokoeni maskini na muhitaji; watoeni mkononi mwa waovu.
Hawajui wala hawaelewi; hutembea gizani; misingi yote ya nchi imebomoka.
Mimi nilisema, “Ninyi ni miungu, na ninyi nyote wana wa Mungu aliye Juu.
Hata hivyo mtakufa kama wanadamu na mtaanguka kama mmoja wa wakuu.”
Uinuke, Ee Mungu, uihukumu nchi, maana unaurithi katika mataifa yote.