Biblia kwa picha

Nyumbani › Agano la Kale › Zaburi

Zaburi 87

Maandiko: Biblia Takatifu, Unlocked Literal Bible, © 2019, CC BY-SA 4.0. Vichwa, utangulizi na picha: Imago Biblia.

Picha za sura hii zinakuja hivi karibuni. Kwa sasa, haya ni maandiko kamili.

Mji aliouanzisha umesimama juu ya mlima mtakatifu;

Yahwe anapenda zaidi malango ya Sayuni kuliko mahema yote ya Yakobo.

Mambo matukufu yamesemwa kwako, mji wa Mungu. Selah

Ninataja Rahabu na Babeli kwa wafuasi wangu. Tazama, Filisti, na Tiro, pamoja na Ethiopia nao watasema, 'Huyu alizaliwa humo.'”

Itasemwa juu ya Sayuni, “Kila mmoja wa hawa alizaliwa katika yeye; na yeye Aliye Juu atamuimarisha.

Yahwe anaandika katika kitabau cha sensa ya mataifa, “Huyu alizaliwa humo.” Selah

Hivyo waimbaji na wachezaji kwa pamoja waseme, “chemchem zangu zimo kwako.”