Biblia kwa picha

Nyumbani › Agano la Kale › Mwanzo

Mwanzo 6
Safina ya Nuhu

Sura ya sita inaeleza nchi iliyojaa dhuluma na wanadamu wenye mwelekeo wa uovu, kiasi kwamba Mungu anaamua kuwaangamiza kwa gharika. Lakini Nuhu, mtu mwenye haki, alipata kibali machoni pa Yahwe. Mungu anampa mpango kamili wa safina ili kuokoa familia yake na wanyama, na Nuhu anafanya kila alichoagizwa.

Maandiko: Biblia Takatifu, Unlocked Literal Bible, © 2019, CC BY-SA 4.0. Vichwa, utangulizi na picha: Imago Biblia.

Mistari 1–4

Wanefili

Ikawa wakati watu walipoanza kuongezeka juu ya uso wa nchi na wana wa kike wakazaliwa kwao,

wana wa Mungu walipoona kuwa mabinti wa wanadamu ni wenye kuvutia. waliwachukua kuwa wake zao, kila waliye mchagua.

Yahwe akaema, “ roho yangu haitasalia kwa mwanadamu milele, kwa kuwa wao ni nyama. Wataishi miaka 120.”

Majitu makubwa yalikuwa juu ya uso wa nchi nyakati hizo, na hata baada ya hapo. Hii ilitokea wakati wana wa Mungu walipowaoa binti za wanadamu, na kupata watoto pamoja nao. Hawa walikuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.

Katika mtaa wenye watu wengi wa mji wa kale, wanaume watatu wakubwa sana waliovaa mavazi meusi, wakiwa na mikuki, wanapita kati ya umati unaosogea kwa hofu.

Mistari 5–8

Nuhu alipata kibali

Yahwe akaona kwamba uovu wa watu umezidi katika nchi, na kwamba mawazo ya mioyo yao daima inaelekea tu katika uovu.

Yahwe akajuta kuwa amemuumba mwanadamu juu ya nchi, na ikamuhuzunisha moyo wake.

Kwa hiyo Yahwe akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu ambaye nimemuumba katika uso wa nchi; mwanadamu na wanyama wakubwa, na vitambaavyo na ndege wa angani, kwa kuwa nimehuzunika kuwa nimeviumba.”

Lakini Nuhu akapata neema ya upendeleo machoni pa Yahwe.

Mji mkubwa wenye giza chini ya anga zito; kando, juu ya kilima, mwale wa nuru unaangaza nyumba ya Nuhu peke yake.

Mistari 9–13

Nuhu alienenda na Mungu

Kulikuwa na matukio kumuhusu Nuhu. Nuhu alikuwa mtu mwenye haki, na asiye na lawama miongoni mwa watu wa kipindi chake. Nuhu alitembea na Mungu.

Nuhu akafanyika baba wa wana watatu wa kiume: Shem, Ham na Yafeti.

Nchi iliharibika mbele za Mungu, na ikajaa ghasia.

Mungu akaiona nchi; tazama, ilikuwa imeharibika, kwa kuwa wote wenye mwili walikuwa wameharibu njia zao juu ya nchi.

Mungu akamwambia Nuhu, “Nimeona kuwa sasa niwakati wa mwisho kwa wote wenye mwili, kwa kuwa inchi imejaa ghasia kutokana na wao. Hakika, nitawaharibu wao pamoja na nchi.

Usiku chini ya nyota, Nuhu amesimama peke yake juu ya kilima, mikono wazi, upepo ukipuliza joho lake; chini kuna taa za mji zenye msukosuko.

Mistari 14–16

Mpango wa safina

Tengeneza safina ya mti wa mvinje kwa ajili yako. Tengeneza vyumba katika safina, na vifunike kwa lami ndani na nje.

Hivi ndivyo utakavyofanya: urefu wa safina dhiraa miatatu, upana wake dhiraa hamsini, kwenda juu kwake dhiraa thelathini.

Tengeneza paa la safina, na ulimalize kwa kipimo cha dhiraa kutoka juu ubavuni. Weka mlango katika ubavu wa safina na utengeneze dari ya chini, ya pili na ya tatu.

Mchoro wa ndani wa safina: sanduku kubwa la mbao lenye umbo la mstatili, lenye dari tatu zilizogawanywa vyumba, mlango ubavuni na tundu chini ya paa. Urefu: dhiraa 300 (≈ m 135) Kimo: dhiraa 30 (≈ m 13) Upana: dhiraa 50 (≈ m 22) Paa na tundu la mwanga (mst. 16) Mlango ubavuni (mst. 16) Vyumba (mst. 14) Dari tatu (mst. 16) Imepakwa lami (mst. 14)

Mistari 17–21

Agano

Sikiliza, nimekaribia kuleta gharika ya maji juu ya nchi, kuharibu wenye mwili wote wakaao ndani ya nchi wenye pumzi ya uhai chini ya mbingu. Kila kitu kilichopo juu ya nchi kitakufa.

Lakini nitalifanya thabiti agano langu na wewe. Utaingia ndani ya safina, wewe, na wana wako wa kiume, na mke wako, pamoja na wake za wanao.

Kwa kila kiumbe hai chenye mwili, viwili vya kila aina utavileta ndani ya safina, ili visalie hai pamoja nawe, vya kike na vya kiume.

Katika ndege kwa jinsi yake, na wanyama wakubwa kwa jinsi yake, kila kitambaacho ardhini kwa jinsi yake, viwili viwili vya kila aina vitakuja kwako ili viwe salama.

Kusanya kila aina ya chakula kinacholiwa kwa ajili yako na ukitunze, ili kwamba viwe chakula chako na chao.”

Mbele ya safina, familia ya Nuhu inapandisha chakula kwa njia ya mteremko; kwa mbali wanyama wanakuja wawili wawili.

Mstari wa 22

“Nuhu akafanya hivi”

Kwa hiyo Nuhu akafanya hivi. kulingana na yote ambayo Mungu alimuagiza, ndivyo alifanya.

Nuhu na wanawe wanajenga safina: mmoja amebeba boriti, mwingine anagongelea vigingi, wa tatu anapaka lami kwenye kiunzi.