Biblia kwa picha

Nyumbani › Agano la Kale › Mwanzo

Mwanzo 5
Kutoka Adamu hadi Nuhu

Sura ya tano ni “orodha ya vizazi vya Adamu”: vizazi kumi kutoka Adamu hadi Nuhu, kila kimoja kikielezwa kwa maneno yale yale hadi “kisha akafa”. Ni mmoja tu anayevunja mdundo huu: Henoko, “aliyeenenda na Mungu” na hakufa. Sura inamalizika kwa Nuhu na wanawe watatu.

Maandiko: Biblia Takatifu, Unlocked Literal Bible, © 2019, CC BY-SA 4.0. Vichwa, utangulizi na picha: Imago Biblia.

Mistari 1 na 2

Orodha ya vizazi vya Adamu

Hii ni orodha ya vizazi vya Adamu. Katika siku ambayo Mungu alimuumba mtu, aliwaumba katika mfano wake mwenyewe.

Mwanaume na mwanamke aliwaumba. Akawabariki na akawaita Adam wakati walipoumbwa.

Mti wa ukoo uliochorwa: tawi la mzeituni linaunganisha duara kumi zenye picha kutoka Adamu hadi Nuhu, kisha linagawanyika kuwa duara tatu ndogo za wanawe.
  1. Adamu · miaka 930
  2. Sethi · miaka 912
  3. Enoshi · miaka 905
  4. Kenani · miaka 910
  5. Mahalaleli · miaka 895
  6. Yaredi · miaka 962
  7. Henoko · miaka 365, Mungu alimtwaa
  8. Methusela · miaka 969
  9. Lameki · miaka 777
  10. Nuhu
  11. Shemu
  12. Hamu
  13. Yafethi

Mistari 3–5

Adamu na Sethi, “katika sura yake”

Wakati Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, akamzaa mwana katika sura yake mwenyewe, kwa mfano wake, na akamuita jina lake Sethi.

Baada ya Adamu kumzaa Sethi, aliishi miaka mia nane. Akawazaa wana wengi waume na wake.

Adamu akaishi miaka 930 kisha akafariki.

Adamu mzee sana ameketi mbele ya nyumba yake jua likizama, mkono wake juu ya bega la mwanawe Sethi anayefanana naye, akizungukwa na wazao wengi.

Mistari 6–20

Kizazi baada ya kizazi

Wakati Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.

Baada ya kumzaa Enoshi, akaishi miaka 807 na akawazaa wana wengi waume na wake.

Sethi akaishi miaka 912 kisha akafariki.

Wakati Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani.

Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815. Akazaa wana wengi wa ume na wake.

Enoshi aliishi miaka 905 na kisha akafariki.

Wakati Kanani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.

Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.

Kenani aliishi miaka 910, na kisha akafariki.

Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, alimzaa Yaredi.

Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830. Akazaa wana wengi wa ume na wake.

Mahalaleli aliishi miaka 895 na kisha akafariki.

Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, alimzaa Henoko.

Baada ya kumzaa Henoko, Yaredi aliishi miaka mianane. Akazaa wana wengi waume na wake.

Yaredi aliishi miaka 962 na kisha akafariki.

Vizazi kadhaa chini ya mzeituni mkubwa: babu mwenye nywele nyeupe anambariki mwanawe aliyepiga magoti huku watoto wakicheza; kijiji kimeenea bondeni.

Mistari 21–24

Henoko aliyeenenda na Mungu

Henoko alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, akamzaa Methusela.

Henoko akaenenda na Mungu miaka miatatu baada ya kumzaa Methusela. Aliwazaa wana wengi wa ume na wake.

Henoko aliishi miaka 365.

Henoko alienenda na Mungu, na kisha alitoweka, kwa kuwa Mungu alimtwaa.

Henoko anatembea peke yake kwenye njia inayopanda kuelekea nuru kubwa ya dhahabu; chini kabisa kijiji chake na familia yake vinaonekana vidogo sana.

Mistari 25–31

“Huyu atatupatia pumziko”

Wakati Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, alimzaa Lameki.

Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.

Methusela aliishi miaka 969. Kisha akafariki.

Wakati Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana.

Akamuita jina lake Nuhu, akisema, “Huyu ndiye atatupatia pumziko kutoka katika kazi yetu na kutoka katika kazi ya taabu ya mikono yetu, ambayo lazima tuifanye kwa sababu ya ardhi ambayo Yahwe ameilaani.”

Lameki aliishi miaka 595 baada ya kumzaa baba wa Nuhu. Akazaa wanawengi wa ume na wake.

Lameki aliishi miaka 777. Kisha akafariki.

Lameki amembeba mwanawe mchanga Nuhu karibu na mke wake, akitazamwa na Methusela mzee sana; mlangoni linaonekana shamba la mawe, miiba na jembe la zamani.

Mstari wa 32

Nuhu na wanawe watatu

Baada ya Nuhu kuishi miaka miatano, akamzaa Shemu, Hamu, na Yafethi.

Nuhu mwenye ndevu za mvi anawakumbatia wanawe watatu, Shemu, Hamu na Yafethi, bondeni; kwa mbali mawingu mazito ya kijivu yanakusanyika.