Biblia kwa picha

Nyumbani › Agano la Kale › Mwanzo

Mwanzo 20
Abraham na Abimeleki

Sura ya ishirini inatokea Gerari, upande wa kusini. Abraham anasema Sara ni dada yake, na mfalme Abimeleki anamchukua. Lakini Mungu anamwonya mfalme katika ndoto; Abimeleki anamrudisha Sara kwa Abraham pamoja na zawadi, na Abraham anamwombea yeye na nyumba yake.

Maandiko: Biblia Takatifu, Unlocked Literal Bible, © 2019, CC BY-SA 4.0. Vichwa, utangulizi na picha: Imago Biblia.

Mistari 1 na 2

Sara anachukuliwa Gerari

Abraham akasafiri kutoka pale hadi nchi ya Negebu, na akakaa kati ya Kadeshi na Shuri. Akawa mgeni akiishi Gerari.

Abraham akasema kususu mkewe Sara, “ni dada yangu.” Kwa hiyo Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma watu wake kumchukua Sara.

Mbele ya kuta za Gerari, maafisa wawili wa mfalme wanamwongoza Sara kuelekea lango la mji, huku Abraham akiwatazama kwa wasiwasi kutoka hemani mwake.

Mistari 3–7

Ndoto ya Abimeleki

Lakini Mungu akamtokea Abimeleki usiku katika ndoto, akamwambia, “Tazama, wewe ni mfu kutokana na mwanamke uliye mchukua, kwa kuwa ni mke wa mtu.”

Basi Abimeleki alikuwa bado hajamkaribia hivyo akasema, “Bwana, Je utaua hata taifa lenye haki?

Je si yeye mwenyewe aliye niambia, 'Sara ni dada yangu?' Hata Sara mwenyewe alisema, 'ni kaka yangu.' Nimefanya hili katika uadilifu wa moyo wangu na katika mikono isiyo na hatia.”

Kisha Mungu akasema naye katika ndoto, “Kweli, ninajua pia kwamba umefanya hili katika uadilifu wa moyo wako, na pia nilikuzuia usitende dhambi dhidi yangu mimi. Ndiyo maana sikuruhusu umshike.

Kwa hiyo, mrudishe huyo mke wa mtu, kwa kuwa ni nabii. Atakuombea, na utaishi. Lakini usipo mrudisha, ujuwe kwamba wewe pamoja na wote walio wa kwako mtakufa hakika.

Usiku chumbani mwake, mfalme Abimeleki anainuka kitandani kwa hofu, mikono juu, katika mwale wa nuru; taji yake iko mezani karibu na taa.

Mistari 8–13

“Umetutendea nini?”

Abimeleki akaamka asubuhi na mapema akawaita watumishi wake wote waje kwake. Akawasimulia mambo haya yote, na watu wale wakaogopa sana.

Kisha Abimeleki akamwita Abraham na kumwambia, “Umetufanyia jambo gani? Ni kwa jinsi gani nimekutenda dhambi kwamba umeniletea mimi na ufalme wangu dhambi hii kubwa? Umenifanyia mimi jambo ambalo halipaswi kufanywa.”

Abimeleki akamwambia Abraham, “Nini kilikushawishi wewe kutenda jambo hili?”

Abraham akasema, “Ni kwasababu nilifikiri hakika hakuna hofu ya Mungu katika sehemu hii, na kwamba wataniua kwa ajili ya mke wangu.'

Licha ya kwamba kweli ni dada yangu, binti wa baba yangu, ingawa si binti wa mama yangu; na ndiye alifanyika kuwa mke wangu.

Wakati Mungu aliponiondoa katika nyumba ya baba yangu na kusafiri kutoka mahali kwenda mahali pengine, nilimwambia mke wangu, kwa kila sehemu tutakayo kwenda, unioneshe uaminifu wako kama mke wangu: Kila mahali tutakapo kwenda, useme juu yangu kuwa, “Ni kaka yangu.”'''

Katika ukumbi wa jumba la kifalme, Abimeleki kwa mikono wazi anamhoji Abraham, anayeinamisha kichwa akiweka mkono moyoni; watumishi wa mfalme wanasikiliza kwa wasiwasi.

Mistari 14–16

Sara anarudishwa kwa Abraham

Ndipo Abimeleki akatwaa kondoo, maksai, watumwa wa kiume na wa kike akampatia Abraham. Basi Abimeleki akamrudisha Sara, mke wa Abraham.

Abimeleki akasema, Tazama, Nchi yangu i mbele yako. Kaa mahali utakapopendezewa.”

Na kwa Sara akasema, Tazama, nimempatia kaka yako vipande elfu vya fedha. Navyo ni kwa ajili ya kufunika kosa lolote dhidi yako machoni pa wote walio pamoja na wewe, na mbele ya kila mtu ambaye umemfanya kuwa na haki.”

Mbele ya jumba la kifalme, Abimeleki anamrudisha Sara kwa Abraham, anayemnyooshea mikono; mtumishi analeta mfuko wa fedha, na ng'ombe na kondoo wanaletwa.

Mistari 17 na 18

Maombi ya Abraham

Kisha Abraham akaomba kwa Mungu, Na Mungu akamponya Abimeleki, mkewe, na watumwa wake wa kike kiasi kwamba wakaweza kupata watoto.

Kwa kuwa Yahwe alikuwa amewafanya wanawake wote wa nyumaba ya Abimeleki kuwa tasa kabisa, kwa sababu ya Sara, mke wa Abraham.

Uwanjani mwa jumba la kifalme, Abraham amepiga magoti juu ya zulia akiomba kwa mikono iliyoinuliwa mbele ya Abimeleki, mke wake na wajakazi wake walioinamisha vichwa.