Biblia kwa picha

Nyumbani › Agano la Kale › Mwanzo

Mwanzo 16
Hajiri na Ishmaeli

Sura ya kumi na sita inasimulia jinsi Sarai, ambaye hana watoto, anavyompa Abram mtumishi wake Mmisri, Hajiri. Hajiri anapopata mimba anamdharau bibi yake, kisha anakimbilia jangwani. Huko, karibu na chemichemi, malaika wa Yahwe anamkuta na kumtangazia kuzaliwa kwa Ishmaeli: Hajiri anamjua Mungu anayemwona.

Maandiko: Biblia Takatifu, Unlocked Literal Bible, © 2019, CC BY-SA 4.0. Vichwa, utangulizi na picha: Imago Biblia.

Mistari 1–3

Sarai anampa Abram Hajiri

Kisha Sarai mke wa Abram, alikuwa hajamzalia mtoto, lakini alikuwa na mtumishi wa kike, Mmisri ambaye jina lake aliitwa Hajiri.

Kwa hiyo Sarai akamwambia Abram, “Tazama, Yahwe hajanifanya mimi kuwa na watoto. Nenda na ulale na mtumishi wangu. Ili kwamba niweze kupata watoto kupitia yeye.” Abram akasikiliza sauti ya Sarai.

Ilikuwa baada ya Abram kuishi miaka kumi katika nchi ya Kanaani ndipo Sarai, mke wa Abram, alimtoa Hajiri yule mmisri mtumishi wake kwa mume wake awe kama mke wake.

Mbele ya hema, Sarai mwenye huzuni anamtambulisha kwa mkono mtumishi kijana Hajiri, aliyeinamisha macho, kwa Abram aliyeketi kwenye kigoda.

Mistari 4 na 5

Dharau ya Hajiri

Kwa hiyo akawa na mahusiano na Hajiri, na akabeba mimba. Na alipoona kuwa amebeba mimba, akamdharau bibi yake.

Kisha Sarai akamwambia Abram, “Jambo hili baya kwangu ni kwa sababu yako. Nilimtoa mtumishi wangu wa kike katika kumbatio lako. Na alipoona kuwa amebeba mimba, nilidharaulika machoni pake. Na sasa acha Yahwe aamuwe kati yangu na wewe.”

Sarai aliyeumizwa anaongea kwa ukali na Abram, anayeinua mikono bila msaada, huku Hajiri mwenye mimba akigeuka kwa kiburi; watumishi wa kike wanatazama.

Mstari wa 6

Hajiri anakimbia

Lakini Abram akamwambia Sarai, “Tazama, hapa, mtumishi wako yuko katika uwezo wako, fanya unachofikiri ni kizuri sana kwake.” Kwa hiyo Sarai akakabiliana naye kwa ukatili, na akatoroka.

Hajiri anaondoka haraka kambini kwenye njia ya mawe, akiwa na kiriba na mfuko begani, akigeuka nyuma kwa hofu; Sarai amesimama mbele ya hema.

Mistari 7–14

“Wewe ni Mungu unionaye mimi”

Malaika wa Yahwe akamkuta karibu na chemichemi ya maji katika jangwa, chemichemi iliyo katika njia kuelekea Shuri.

Akasema, Hajiri, mtumishi wa Sarai, umetoka wapi na unakwenda wapi?” Na akasema, ninamtoroka bibi yangu Sarai.”

Malaika wa Yahwe akamwambia, “ Rudi kwa bibi yako, na unyenyekee chini ya mamlaka yake.”

Kisha Malaika wa Yahwe akamwambia, “Nitazidisha uzao wako maradufu, kiasi kwamba watakuwa wengi wasioweza kuhesabika.”

Malaika wa Yahwe pia akamwambia, “ Tazama, wewe unamimba, na utazaa mtoto kiume, na utamwita jina lake Ishmaeli, kwasabab Yahwe amesikia mateso yako.

Atakuwa punda mwitu wa mtu. Atakuwa adui dhidi ya kila mtu, na kila mtu atakuwa adui yake, na ataishi kando na ndugu zake wote.”

Kisha akamwita jina hili Yahwe aliye zungumza naye, “Wewe ni Mungu unionaye mimi,” kwa kuwa alisema, “je ninaendelea kweli kuona, hata baada ya kuwa ameniona?”

Kwa hiyo kisima kiliitwa Beerlahairori; Tazama, kiko kati ya Kadeshi na Beredi.

Jangwani, Hajiri amepiga magoti karibu na chemichemi chini ya mitende na kuinua macho kuelekea nuru inayoshuka juu yake.

Mistari 15 na 16

Kuzaliwa kwa Ishmaeli

Hajiri akamzalia Abram mwana wa kiume, na Abram akamwita mwanawe, ambaye Hajiri amemzaa jina, Ishmaeli.

Abram alikuwa na umri wa miaka themanini na sita wakati Hajiri alipomzaa Ishmaeli kwa Abram.

Ndani ya hema, Abram amembeba mtoto mchanga karibu na Hajiri anayetabasamu; mtumishi analeta bakuli, na Sarai anatazama kutoka mlangoni.